Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema mabingwa hao wa nchi wanahitaji kupata ushindi dhidi ya Al Merrikh ili kijiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali
Akizungumza na wanahabari leo kuelekea mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa kumi jioni, Gomes amesema ili Simba iweze kutinga robo fainali, inahitaji kufikisha alama 11
"Tutafanya mabadiliko kidogo ya kikosi. Tunahitaji kushinda mchezo huu hivyo tunahitaji kushambulia"
"Ili tuweze kufuzu hatua inayofuata tunapaswa kufikisha alama 11, hivyo mchezo huu tunapaswa kushinda," alisema Gomes
Aidha Gomes amesema beki Paschal Wawa ndiye mchezaji pekee ambaye hatakuwa sehemu ya kikosi kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano
ADVERTISE HERE