Simba yatahadharishwa mechi dhidi ya Al Merrikh

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Mar 2021
Simba yatahadharishwa mechi dhidi ya Al Merrikh

Nyota wa zamani wa Simba Amir Kiemba ambaye sasa  ni mchambuzi mahiri wa soka, amesema Simba inapaswa kujipanga kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Al Merrikh kwani ni wazi kama hawatapata matokeo mechi mbili zitakazobaki zitakuwa ngumu zaidi

Kiemba amesema kuna kila dalili nguvu za ziada zimeanza kutumika kuhakikisha Simba haisongi mbele baada ya kufanya vizuri mechi zake za mwanzo na kuwaweka kwenye hatihati ya kuwania nafasi moja ya kufuzu vigogo Al Ahly na AS Vita

"Kwa namna ambavyo Kundi A linakwenda, inaonekana kama Simba imevuruga matokeo ambayo tayari yalishakuwepo kwenye makaratasi"

"Kwa sababu baada ya kundi kupangwa, kuna timu ambazo tayari watu walikuwa wanafikiria zitafuzu. Kuna msemo unasema, ukiomba mafanikio ujue maadui wanaongezeka. Kwa hiyo sasa hivi maadui wa Simba wameongezeka na wanataka kuhakikisha ile nafasi yao inapotea"

"Nafikiri hata kuzuia mashabiki ni njia ya kuivuruga timu na uongozi kwa ujumla. Sasa hivi vita imeshakuwa kubwa, hata mechi ya kesho naona Simba inacheza na kundi zima sio na Al Merrikh peke ake"

"Kwa hiyo naiona ni mechi ngumu sana nje na ndani ya uwanja. Kwa hiyo viongozi na timu kwa ujumla wanatikiwa kuiendea mechi hii kwa tahadhari kubwa kuliko hata walivyokuwa wanachukulia mechi zilizopita," alisema Kiemba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’