Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa mchezo wa raundi ya nne ligi ya mabingwa dhidi ya El Merrikh, anakusudia kubadili mbinu ili kuweka mazingira bora ya kuweza kupata pointi tatu.
Gomes amesema wanafanya maandalizi tofauti kwani hata wachezaji ambao walitumika kwenye mchezo wa kwanza wanatakiwa kuongezewa nguvu ya wachezaji wengine ambao walikuwa nje ya uwanja.
Mfaransa huyo amesema wachezaji wa Al Merrikh wana nguvu kubwa na kasi hivyo wachezaji wake wanatakiwa kuanza mashambulizi kuanzia nyuma na kwenda mbele huku wakiwa na nidhamu kubwa ya ukabaji
"Huo ni mchezo muhimu sana kwetu kwa sababu ndiyo utarahisisha kazi yetu ya kwenda kucheza kwenye hatua inayofuta"
"Al Merrikh kila mmoja aliwaona namna ambavyo wanacheza kwa kasi na nguvu kubwa, timu yangu inatakiwa ilitambue hilo"
"Bahati kwamba kila mmoja anatambua umuhimu wa kupata pointi tatu kwenye mchezo huo. Tutaongeza nguvu ya kucheza kuanzia nyuma kwenda mbele na bila shaka tutafanikiwa,” amesema Gomes.
Simba walitoka suluhu kwenye mchezo uliopigwa Sudan na keshokutwa Jumanne watakutana tena kwenye mchezo wa raundi ya nne utakaochezwa jijini Dar es salaam, kwenye Uwanja wa
Mchezo huo utachezwa bila ya uwepo wa mashabiki kutokana na Shirikisho la Soka Afrika, (CAF) kutoa zuio hilo