Mkude kamili kuwavaa El Merrikh

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Mar 2021
Mkude kamili kuwavaa El Merrikh

Kiungo Jonas Mkude keshokutwa anatarajiwa kurejea katika kikosi wakati Simba itakaposhuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili El Merrikh katika mchezo wa ligi ya mabingwa raundi ya nne

Tangu akumbane na adhabu iliyosababishwa na utovu wa nidhamu mwishoni mwa mwaka uliopita, Mkude amepoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza kwa Taddeo Lwanga aliyetua kwenye usajili wa dirisha dogo

Hata hivyo Lwanga atakosa mchezo dhidi ya El Merrikh kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano

Yeye pamoja na beki Paschal Wawa hawatakuwa sehemu ya mchezo huo sababu ya kadi

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes alisema hana wasiwasi na Mkude, anaweza kutekeleza majukumu yaliyokuwa yakifanywa na Lwanga bila ya wasiwasi

Katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons, Mkude alianza sambamba na Mzamiru Yassin ambaye pia amejihakikishia nafasi kwenye kikosi cha Gomes

Huu utakuwa mchezo wake wa kwanza katika michuano ya ligi ya mabingwa mwaka huu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’