Mechi dhidi ya El Merrikh kuchezwa bila ya mashabiki

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Mar 2021
Mechi dhidi ya El Merrikh kuchezwa bila ya mashabiki

Mchezo wa raundi ya nne michuano ya ligi ya mabingwa kati ya Simba dhidi ya El Merrikh ambao utapigwa Jumanne, March 16, hautahudhuriwa na mashabiki

Mkuu wa idara ya habari na Mawasiliano klabu ya Simba, Haji Manara amesema wamepokea maagizo ya CAF kupitia TFF mapema leo wakati wakiendelea na maandalizi ya mchezo huo

"Mechi yetu na Al Merrikh ipo pale pale lakini wakati tukiendelea na maandalizi tumepokea taarifa kutoka TFF ambayo imetolewa na CAF kwamba tucheze bila mashabiki."

"Mnawajua mashabiki wetu lakini hakuna namna tutacheza bila mashabiki. Wanaruhusiwa maafisa na watu wachache ambao wanahusika na mchezo."

"Simba imezoea kucheza bila mashabiki ikiwa nje ya nchi lakini sikumbuki kama hapa nchini tumewahi kucheza bila mashabiki. Tunawaomba radhi mashabiki kwa mechi hii sababu ni maamuzi ya CAF ambao ndio wenye mamlaka ya soka Afrika."

"Itakuwa ni vita ya kimya kimya kama ambavyo Simba anawinda. Wachezaji wetu wamezoea kucheza mbele ya mashabiki na wamezoea kucheza bila mashabiki, naamini wana uzoefu wa kutosha kucheza kwenye hali kama hiyo."

"Wanachoweza kufanya kwasasa mashabiki ni kuwaombea wachezaji na kuwaonyesha wachezaji hatupo uwanjani lakini tunawaombea na kuwapa nguvu," alisema Manara

Aidha 'Bugati' amesisitiza kuwa katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu, wamekusudia kufanya jambo kubwa ambalo litaipa Simba na Tanzania heshima kubwa

"Simba imekusudia na inayo dhamira kuhakikisha mwaka huu tunafanya jambo kubwa ambalo litatupa heshima tunayostahili kama SIMBA."

"Tumepanga kufanya makubwa zaidi ya lengo la kufika nusu fainali. Tunakwenda kwenye mikakati mikubwa."

"CEO Barbara anapokwenda kwenye mikutano mikubwa kuna jambo kule. Sisi tunakwenda kwenye NEXT LEVEL. Tunajenga furaha ya miaka," aliongeza Manara

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
4h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
10h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’