Wapinzani wa Simba, klabu ya El Merrikh imeondoka nchini Sudan kuja Tanzania tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa utakaopigwa Jumanne,March 16 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Kupitia ukurasa wao wa mtandao wa kijamii, El Merrikh wamethibitisha ujio wa timu yao Tanzania kwa ajili ya mchezo huo
Timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana katika mchezo wa raundi ya tatu uliopigwa nchini Sudan
Mabingwa wa nchi Simba watahitaji kushinda mchezo wa Jumanne ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali wakati wakisubiri hatma ya rufaa waliyokata CAF kupinga El Merrikh kuchezesha wachezaji wawili waliofungiwa katika mchezo uliopita
ADVERTISE HERE