Mshambuliaji wa Simba Queens Mwanahamisi 'Gaucho' anaelekea nchini Morocco kujiunga na klabu ya Chabab Atlas Women FC inayoshiriki ligi kuu ya Wanawake nchini humo
Mwanahamisi ambaye ni nahodha wa Simba Queens anakuwa mchezaji wa kwanza ligi kuu ya Wanawake nchini kupata timu nje ya nchi
Hii ni hatua kubwa sana kwa Ligi Kuu ya Wanawake ambayo ndio kwanza imeingia msimu wa nne hapa Tanzania
Kwa Simba Queens huu ni mwanzo tu, bila shaka Simba kama klabu itanufaika kwa kuwauza wachezaji zaidi nje ya nchi huku ikiendelea na utaratibu wake wa kusajili wachezaji wenye vipaji
ADVERTISE HERE