Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa ' , Kim Poulsen amesema wachezaji wa Simba Sc walioitwa timu ya Taifa wataungana na timu hiyo nchini Kenya mara baada ya kumaliza majukumu yao ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya El Merrikh
Simba itacheza na El Marrikh Jumanne, March 16 katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Nyota wa Simba walioitwa timu ya Taifa ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Kennedy Juma, Mohamed Hussein, Hassan Dilunga, Jonas Mkude, Said Ndemla,, John Bocco na Mzamiru Yasin
Stars itacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Harambee Stars March 15 na March 18 nchini Kenya
ADVERTISE HERE