Al Masry ndio saizi yetu - Manula

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
24 Feb 2018
Al Masry ndio saizi yetu - Manula
Simba imewaondoa Gendarmarie ya Djibouti na sasa itakutana na Al Masry ya Misri kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Mchezo kwanza unatarajiwa kupigwa Ijumaa ya March 09 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kuelekea mchezo huo, Mlinda lango namba moja Tanzania, Aishi Manula amefurahishwa na ratiba ya kukutana na Al Masry kwa kuwa anaamini hao ndiyo ‘saizi’ yao kutokana na ubora wa kikosi cha Simba sasa.

Simba ilifanikiwa kutinga katika hatua ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuwaondoa Gendarmarie kwa ushindi wa mabao 5-0 walioupata nyumbani na ugenini.

Timu hiyo, katika uwanja wake wa nyumbani ilifanikiwa kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya kurudiana ugenini na kushinda bao 1-0.

Manula amefunguka kuwa kwa upande wao wachezaji wamejiandaa vema na mchezo huo na kikubwa malengo yao ni kuwaondoa kuwaondoa Al Masry katika hatua hiyo ya michuano.

Manula alisema, mechi mbili zilizopita walizocheza na Gendarmarie hazikuwa ngumu kulinganisha na ubora wa kikosi chao ambacho kinaundwa na wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa.

“Michezo miwili ya hatua ya awali kwenye Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gendarmarie haikuwa migumu sana kulinganisha na ubora wa kikosi cha Simba.

“Ilikuwa ni michezo ya kawaida sana ila nadhani sasa kwenye mchezo unaofuata ndiyo tunaanza mashindano rasmi na tunajiandaa vyema sana kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Al Masry ambao tutaanza nyumbani kwa kucheza mchezo wa kwanza,” amesema Manula.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3m ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →