Gomes ataja sababu ya kutowatumia Lokosa, Muduhwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Mar 2021
Gomes ataja sababu ya kutowatumia Lokosa, Muduhwa

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema hana shaka na uwezo wa beki Peter Muduhwa katika viwanja vya mazoezi na anaamini wakati wake wa kupata nafasi utafika

Hata hivyo amesema kwa sasa hawezi kumtumia mshambuliaji Junior Lokosa kwa kuwa hayuko fiti

Lokosa na Muduhwa waliongezwa kwenye kikosi cha Simba katika usajili wa dirisha dogo kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa

Hata hivyo wawili hao wamekuwa na wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba

Gomes amefunguka sababu ya kutowatumia wachezaji hao

"Lokosa hakucheza mechi zenye ushindani kwa muda mrefu kutokana na kule alikokuwa ligi haikuwepo kwa sababu ya corona, kwahiyo mpaka muda anafika hapa hakuwa na utimamu wa mwil"

"Nahitaji muda zaidi wa kumtengeneza Lokosa na kurudisha utimamu wake wa mwili na baada ya hapo ndio nimpatie nafasi ya kucheza, ndio maana mpaka sasa hajaonekana katika mechi za mashindano," Gomes amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

"Muduhwa amekuwa akifanya vizuri hata mazoezini lakini inakuwa ngumu kupangua wachezaji ambao wanacheza vizuri na kuelewana katika ligi lakini kama itatokea changamoto au mahitaji zaidi nafasi ya kucheza inawezekana"

"Baada ya msimu kumalizika tutafanya tathmini ya kikosi kizima na kuangalia mahitaji ya timu yetu baada ya hapo ndio nitatoa mtazamo wangu wachezaji ambao tunatakiwa kubaki nao na maeneo ya kuongeza nguvu"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’