Gomes ataka umakini safu ya ushambuliaji

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Mar 2021
Gomes ataka umakini safu ya ushambuliaji

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jana usiku

Mchezo huo ulishuhudia maafande wa Tanzania Prisons wakipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba

Akizungumza baada ya mchezo huo, Gomes alisema walitengeneza nafasi nyingi lakini hawakuwa makini katika umaliziaji

Kocha huyo raia wa Ufaransa alisema wanahitaji kufanyia kazi kutumia nafasi za mipira ya adhabu kwani hawana uwiano mzuri wa kufunga mabao kupitia mipira hiyo

Mshambuliaji Chris Mugalu alikosa mkwaju wa penati, akiungana na Meddie Kagere ambaye pia alikosa katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya African Lyon

"Tunahitaji kufanyia kazi eneo letu la ushambuliaji hasa matumizi ya mipira ya adhabu. Nafikiri hatukuwa makini kwa ujumla"

"Tulikuwa na changamoto kwenye safu ya ulinzi lakini kwa sasa tuko sawa, nafurahia kuona hatufanyi makosa mengi"

"Tumekubali matokeo, tunajipanga kwa mchezo ujao, ligi bado ni ndefu bado kuna mechi nyingi mbele yetu," alisema Gomes

Baada ya mchezo huo Simba inahamishia nguvu zake kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ambapo Jumanne ijayo watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikaribisha Al Merrikh katika mchezo muhimu ambao Simba inahitaji ushindi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’