Simba kuivaa Mbao FC kwa tahadhari kubwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Feb 2018
Simba kuivaa Mbao FC kwa tahadhari kubwa
Mbao FC ilikuwa timu ya kwanza kufunga goli dhidi ya Simba tangu kuanza kwa msimu huu 2017/2018.

Mwanzoni mwa msimu, Simba walimudu kucheza mechi tatu bila kuruhusu bao katika nyavu zao huku Aishi Manula akiwa amecheza kwa zaidi ya dakika 325 bila kufungwa.

Mbao waliibana Simba na kuilazimisha sare ya kufungana 2-2 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika mechi ya mzunguuko wa kwanza.

Timu hizo zinakutana tena keshokutwa Jumatatu kwenye mchezo wa mzunguuko wa pili ligi kuu ya Vodacom, mchezo ukipigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Wakati Simba ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kujikusanyia alama 42, Mbao FC iko nafasi ya 11 ikiwa na alama 19.

Mchezo huo pia utahusisha vita ya wapachika mabao ambapo kinara wa mabao wa Simba Emanuel Okwi ndiye anayeongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu baada ya kufunga mabao 14.

Habibu Kiyombo wa Mbao FC yuko nafasi ya nne nyuma ya John Bocco kwa tofauti ya bao moja akiwa amefunga mabao tisa.

Mchezo huu pia utahusisha timu zinazotumia mfumo wa aina moja (3-5-2). Simba imekuwa ikitumia mfumo huo tangu kocha Msaidizi Masudi Djuma alipokabidhiwa mikoba baada kutimuliwa Omog.

Kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre ameamua kuendeleza mfumo huo huku Mbao FC ikitumia mfumo huo tangu msimu uliopita.

Simba imekuwa na mwenendo mzuri inapocheza uwanja wa nyumbani hivyo kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Hata hivyo Mbao FC inatarajiwa kutoa upinzani mkali kwa kuwa inaweza kuingia kwenye hatari ya kushuka daraja kama itapoteza mchezo huo.

Kwani ina tofauti ya alama nne tuu dhidi ya timu zilizo mkiani, Kagera Sugar Majimaji na Njombe Mji ambazo zote zina alama 15.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
10m ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
32m ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
3h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
23h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’