Gomes azitaka alama tatu mechi ya Prisons

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Mar 2021
Gomes azitaka alama tatu mechi ya Prisons

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes, amesema licha ya kuwaheshimu wapinzani wake katika mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kesho Jumatano, anaamini kikosi chake kitaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Simba inaingia katika mchezo huu ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya JKT Tanzania

Gomes amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo na lengo lao ni kuhakikisha wanashinda ili kuongeza alama ambazo zitawasogeza karibu na uongozi wa ligi

"Kikosi chetu kiko tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons, tunajua hautakuwa mchezo rahisi kutokana na uhalisia wa timu ambayo tunakwenda kucheza nayo"

"Simba ilipoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya timu hii, na hivyo tunapaswa kuwa makini zaidi dhidi yao kwani hiyo inaonyesha ni kwa kiasi gani wana timu ambayo inaweza kupambana"

"Lakini matokeo ya ushindi katika mchezo huu ni ya muhimu kwetu, tunapaswa kushinda ili kuendelea kuusogelea zaidi uongozi wa ligi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Yanga," amesema Gomes

Simba iko nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 45 lakini ikiwa imeshuka dimbani mara 19

Mabingwa hao wa nchi wana michezo minne ya viporo, ushindi katika michezo yote utawafanya waongoze ligi kwa tofauti ya alama saba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’