Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage amefafanua namna ambavyo Simba inaweza kunufaika baada ya klabu ya Al Merrikh kuwatumia wachezaji waliofungiwa kwenye mchezo uliowakutanisha kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Rage amesema mchezaji hawezi kushiriki mashindano ya CAF kama hana leseni ya kushiriki ligi ya nchi anapocheza
"Timu ya Simba ina nafasi kubwa ya kupata pointi tatu (3) kutoka kwa Al Merrikh kutokana na Al Merrikh kuwatumia wachezaji watatu ambao hawakupaswa kucheza katika mchezo baina ya timu hizo uliopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Sudan"
"Wachezaji hao wamefungiwa na Chama cha Mpira cha Sudan baada ya kufanya kosa la kusaini vilabu viwili tofauti"
"Kulingana na barua ambayo Chama cha soka cha Sudan kimeviandikia vilabu kuwajulisha wamewafungia wachezaji hao, kama (SFA) waliomba baraka za CAF na FIFA, moja kwa moja wachezaji hao wanakosa sifa kucheza mashindano ya kimataifa"
"Simba wanao mwanya mwingine wa kisheria wakiutumia nadhani watakuwa na nafasi ya kushinda rufaa yao"
"Ile adhabu ambayo wamepewa wachezaji wa Al Merrikh wamepoteza sifa ya kuwa wachezaji wa ligi ya Sudan. Kwakuwa wamepoteza sifa ya kuwa wachezaji wa Sudan lakini sheria za CAF (sheria namba 5 ya usajili) ili mchezaji aruhusiwe kushiriki mashindano ya CAF lazima awe na leseni ya kucheza mashindano ya ndani," alisema Rage
Simba inaongoza kundi A michuano ya ligi ya mabingwa ikiwa imejikusanyia alama saba
Lakini kama rufaa yao itakubalika na CAF, Simba inaweza kupewa alama zote za mchezo wa kwanza dhidi ya Al Merrikh na hivyo kufikisha alama 9
Kimahesabu watahitaji alama mbili tu kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa