Okwi aikamia Mbao FC

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Feb 2018
Okwi aikamia Mbao FC
Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, Emmanuel Okwi, amesema kikosi chao kinajizatiti kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC na baadaye wataelekeza nguvu kwa wapinzani wao wa Kombe la Shirikisho Afrika, timu ya Al Masry ya Misri.

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba watawakaribisha Mbao katika mchezo wa ligi hiyo utakaofanyika Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Okwi aliyefunga bao pekee kwenye mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya Gendarmerie amesema kuwa kila siku wanajiandaa na kujiimarisha kwa kuzingatia mchezo unaofuata na hiyo ndiyo mbinu sahihi ya kuhakikisha wanapata pointi tatu kila wanaposhuka dimbani.

Okwi amesema kuwa wataikabili Mbao FC bila kujali matokeo ya sare ya mabao 2-2 waliyopata kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza, kwa sababu kila timu inaingia tofauti katika hatua ya lala salama ambayo bingwa na klabu zinazoshuka daraja hujulikana.

"Najua wengi wanaiwaza mechi dhidi ya Al Masry, lakini kumbukeni tunamechi nyingine dhidi ya Mbao kutoka Mwanza, ni mchezo mgumu ambao tunatakiwa kupambana ili tupate pointi tatu na kujiweka katika mazingira bora ya mbio za kuwania ubingwa," Okwi alisema.

Mshambuliaji huyo aliongeza kuwa bado katika mawazo yake hakufikiria kuwaza kuwania kiatu cha dhahabu lakini anafurahi kuona Simba iko kileleni na yeye ndiye anaongoza kwenye safu ya washambuliaji msimu huu.

"Sikupanga kuwania kiatu cha dhahabu, awali malengo yangu yalikuwa ni kuisaidia timu ili kutwaa ubingwa, lakini sasa niko kwenye nafasi hiyo, hivyo naongeza nguvu kuhakikisha pia napata tuzo hiyo kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu," aliongeza Okwi.

Naye Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema kuwa wanawaomba mashabiki wa timu hiyo kuendeleza umoja ili waweze kutimiza malengo yao katika mechi zilizobakia za nyumbani na ugenini.

Baada ya mechi hiyo dhidi ya Mbao FC, Simba itaendelea kukaa jijini Dar es salaam kuwasubiri Stand United kutoka Shinyanga na Machi 9 mwaka huu itawakaribisha Al Masry katika mchezo wa kwanza wa hatua ya kwanza utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.

Nipashe
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’