Klabu ya Simba imepeleka malalamiko kunako shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kufuatia klabu ya Al Marreikh ya Sudan kuwatumia wachezaji waliofungiwa katika mchezo wao wa ligi ya mabingwa uliofanyika siku chache zilizopita
Wachezaji Ramadhan Agab na Bhakit Khamis walifungiwa na chama cha soka Sudan (SFA) kwa muda wa miezi sita kufuatia kusaini mikataba ya kuvitumikia vilabu viwili tofauti vya Al Hilal na Al Marreikh kwa wakati mmoja
Adhabu ya nyota hao inamalizika katikati ya mwezi Aprili 2021,na hawakuwahi kuitumikia Al Marreikh katika mchezo wowote msimu huu kabla hawajacheza mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Simba uliomalizika kwa sare ya bila kufungana
Uongozi wa Simba unazo nakala za uthibitisho wa barua za kifungo cha wachezaji hao, na wamewasilisha ushahidi huo huko CAF
Kama CAF itakubaliana na madai hayo ya Simba, ni wazi mabingwa hao wa nchi watapewa alama tatu na mabao matatu kutoka mchezo uliopigwa nchini Sudan wiki iliyopita na kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana