Tutafika mbali Ligi ya Mabingwa - Kapombe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Mar 2021
Tutafika mbali Ligi ya Mabingwa - Kapombe

Mlinzi wa kulia wa Simba na timu ya Taifa, Shomari Kapombe ametamba kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanafika mbali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Al Merrikh nchini Sudani, Simba imeendelea kuongoza kundi A baada ya kujikusanyia alama saba, alama tatu mbele ya AS Vita na Al Ahly zenye alama nne kila moja

Kapombe amesema mpaka sasa wamekuwa na msimu bora zaidi katika michuano hiyo

Anaamini wakiendelea kujituma watafika mbali sana malengo makuu yakiwa angalau kuvuka hatua ya robo fainali

"Tumekuwa na wakati mzuri msimu huu, ni jambo zuri na la kujivunia kwetu kama timu. Kikosi kimekuwa na ushirikiano mkubwa na bila shaka kuendana na plani ambazo tunazo naamini tutafika mbali katika michuano hii kulinganisha na misimu mingine tuliyoshiriki," alisema Kapombe

Simba itarudiana na Al Merrikh Jumanne ijayo katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Ushindi katika mchezo huo, utaifanya Simba ihitaji alama moja tu kuweza kuvuka hatua ya robo fainali

Mabingwa hao wa nchi wana michezo miwili nyumbani dhidi ya Al Merrikh na AS Vita wakati mchezo wa mwisho watasafiri nchini Misri kuikabili Al Ahly

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’