Baada ya kuitikisa Afrika kwenye michuano ya ligi ya mabingwa wakibaki kuwa timu pekee ambayo haijaruhusu bao kwenye michuano hiyo, Machampioni wa Taifa hili Simba leo wanarejea mazoezini kuanza kuiwinda Tanzania Prisons
Huwezi amini kazi imekuwa rahisi sana kwa Simba kurudi kileleni kwani wanachopaswa kufanya ni kushinda mechi zao nne za viporo na kuongoza ligi kwa tifauti ya alama saba!
Huko kwa jirani wameanza kufukuzana, kuna watu wameanza kutafuta vichaka vya kujificha baada ya kubaini kupambana na mnyama haiwezekani na ni suala la muda tu atarejea katika nafasi yake
Mchezo dhidi ya Prisons utapigwa keshokutwa Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa 'aka Machinjioni'
Hii ni mechi ya kisasi kwa Simba, hawa Prisons walishinda mchezo wa kwanza uliopigwa kule Sumbawanga
Simba ilitua jana kutoka Sudan ambako walifanikiwa kupata matokeo ya suluhu ya bila kufungana dhidi ya Al Merrikh, matokeo ambayo yamewabakisha kileleni mwa kundi A wakiwa na alama zao saba