Kikosi cha Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kimerejea salama jijini Dar es salaam wakitokea Sudan katika mchezo wa ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Merrikh wakifanikiwa kurudi na alama moja baada ya kulazimisha matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Mabingwa hao wa nchi wanakabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa Jumatano March 10, katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Watakuwa na siku mbili za kujiandaa na mchezo huo pomoja na mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh ambao utapigwa March 16
Simba iko kileleni mwa kundi A ikiwa imejikusanyia alama saba baada ya kushuka dimbani mara tatu katika michuano ya ligi ya mabingwa





ADVERTISE HERE