Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara 'Bugati' amemtaka Mwandishi wa Habari mkongwe Maulid Kitenge kuacha kutumika kuandika taarifa za upotoshaji ambazo zina lengo la kuvuruga utulivu ulioko ndani ya klabu ya Simba
Hivi karibuni kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Kitenge aliandika taarifa akidai winga Bernard Morrison haelewani na kocha Didier Gomes baada ya Morrison kugoma kujumuishwa katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya African Lyon
Manara amesema ni kawaida kwa Kitenge kutumia vyombo vya habari anavyofanya kazi kuzusha taarifa zenye lengo ovu dhidi ya Simba
Msemaji huyo wa mabingwa wa nchi amesisitiza kuwa hawatasita kumchukulia hatua kama ataendelea na tabia hiyo
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Manara ameandika haya;
"Tumekuvumilia mara nyingi sana lakini Kwa sasa uvumilivu umetushinda,,
Kwa nn kila siku ni ww tu kuiongopea Simba mambo ya uongo?
Unaitumia mara kadhaa @wasafifm kuelezea migogoro hewa kuhusu Simba na kutaka kuichafua klabu yetu Kwa maslahi yako binafsi!!
Umekuwa ukifanya hvyo hata ktk Wall zako.
Utadhani Wasafi ni redio yako binafsi. Simba haitaki iandikwe na kutangazwa kwa mazuri tu, Waandishi na watangazaji wana haki ya kutukosoa Kwa mabaya pia kama tumeyafanya, lakini haitavumilia tena story za uongo na kutunga ambazo hazina source,na zimejaa uzushi
Ndugu yangu @diamondplatnumz ongea nae huyu mtu, tulio nje tunaona hana nia njema na ustawi wa uwekezaji ulioufanya ,nadhan nia yake ni kuona Wasafi fm inakuwa na ugomvi na Wanasimba, na mimi sitakubali kazi niliyopewa na klabu hii ichafuliwe na mtu huyo huyo kila siku, vinginevyo labda anataka Wanasimba waisuse kusikiliza hii redio,kitu ambacho mimi ntakuwa mtu wa mwisho kukisema ,ukizingatia mahusiano yangu binafsi na wewe.
Lakini akiendelea kututangaza uongo na kuandika uongo juu yetu na wachezaji wetu,zipo hatua‘Makhsuus’tutazichukua!!
Simba ni klabu kubwa mno haiwezi kumuogopa mtu mmoja Kwa chuki zake binafsi kutuchafua kila siku,,
Nipo hapa kuisemea klabu hii na kuitetea Kwa nguvu zangu zote hadi pale ukomo wangu utakapotimia ,,
Na katika kipindi changu mm kama head wa idara ya habari na mawasiliano kwenye klabu hii,,sitakubali story za upumbav na za uongo dhidi yetu Kwa sababu yoyote ile,,Narudia tena hili likijirudia la uongo uongo iwe Kwa wachezaji,makocha au viongozi na hata timu Kuna hatua’ MAKHSUUS’ tutazichukua!!!
Nani miongoni mwetu atakaekubali taasisi anayoingoza ichafuliwe?
Wanasimba hii ngoma kwanza niachieni mm ,,labda huyu mtu hajajua how Simba is BIG
Kaona tunapata matokeo kila mahali na kaona Simba imetulia anaanzisha uongo wake, Safari hii nnae na akibisha aendelee"