Simba yahitaji alama nne robo fainali

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Mar 2021
Simba yahitaji alama nne robo fainali

Al Ahly imelazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya AS Vita katika mchezo wa ligi ya mabingwa raundi ya tatu uliopigwa nchini Misri

Mapema jana Simba ilifanikiwa kupata alama moja nchini Sudan na kufikisha alama saba wakiendelea kubaki kileleni

AS Vita na Al Ahly zinafuata katika nafasi ya pili na ya tatu zote zikiwa na alama nne wakati Al Merrikh wanaburuza mkia wakiwa na alama moja

Kimahesabu Simba inahitaji angalau alama nne kutoka mechi tatu zilizobaki ili iweze kujihakikishia kutinga robo fainali

Mechi mbili dhidi ya Al Merrikh na AS Vita zitachezwa jijini Dar es salaam na mchezo wa mwisho ni dhidi ya Al Ahly kule Misri

Mchezo dhidi ya Al Merrikh ni lazima Simba ishinde na kisha kupigania ushindi au alama moja dhidi ya AS Vita

Kwa jinsi msimamo ulivyo timu zote zina nafasi ya kufuzu kama zitachanga vyema karata zao, silaha muhimu kwa Simba ni mechi hizi mbili za nyumbani

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
54m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’