Match Day : Al Merrikh vs Simba, CAFCL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Mar 2021
Match Day : Al Merrikh vs Simba, CAFCL

Mabingwa wa nchi Simba jioni ya leo wataendelea na majukumu ya kuiwakilisha nchi Kimataifa watakaposhuka dimbani huko Sudan kuikabili Al Merrikh ukiwa ni mchezo wa raundi ya tatu, michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Vijana wa kocha Didier Gomes wanahitaji kushinda mchezo huu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali

Vinara hao wa kundi A, wanafahamu ushindi katika mchezo wa leo na ule wa marudiano ambao utapigwa jijini Dar es salaam siku 10 zijazo, unaweza kutosha kuipeleka Simba robo fainali bila ya kujali matokeo ya mechi mbili zitakazokuwa zimebaki dhidi ya AS Vita na Al Ahly

Mchezo utapigwa kuanzia saa tisa Alasiri kwa saa za Sudan ambako huku Tanzania itakuwa ni saa kumi jioni

Gomes amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo ambao wanatarajia utakuwa na ushindani mkali

Kocha huyo raia wa Ufaransa amesema anawafahamu vizuri Al Merrikh ikiwa ni timu aliyokuwa akiifundisha kabla ya kutua Simba hivyo amewaandaa vijana wake kimbinu kuweza kupata matokeo leo

Naye Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema timu iko kamili kuelekea mchezo huo, amewataka mashabiki wa Simba na Watanzania wazalendo kuwaombea dua kwani ushindi wao ni ushindi wa nchi

Kila la kheri mabingwa, kila la kheri wawakilishi wa nchi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
20h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’