Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema kikosi cha mabingwa hao wa nchi kiko tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh ambao utapigwa kesho Jumamosi nchini Sudan
Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake, Gomes amesema watawakabili kwa tahadhari wapinzani wao kuhakikisha wanapata matokeo muhimu
Amesema anaifahamu vizuri Al Merrikh hivyo wamejiandaa kukabiliana nao kama walivyofanya katika michezo miwili dhidi ya AS Vita na Al Ahly
"Itakuwa mechi ngumu, naijua vizuri Al Merrikh kwahiyo tunawaheshimu lakini tupo tayari kupambana na kuzuia kama tulivyofanya kwa AS Vita Club na kucheza mpira wetu kama tulivyofanya kwa Al Ahly," alisema Gomes
Simba ilitua Sudan Alfajiri ya kuamkia jana, wachezaji wakapata mapumziko na jioni wakashiriki mazoezi yao ya kwanza
Mchezo utapigwa kesho Jumamosi saa kumi Alasiri kwa saa za Tanzania