Baada ya kuishuhudia Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa VPL uliopita, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, ameweka rekodi ya kutopoteza mchezo kwenye mashindano yote kwa dakika 810
Mfaransa huyo alijiunga na Simba mapema mwezi Januari akichukua mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye alitimkia Morocco kwenye Klabu ya Far Rabat
Gomes ameiongoza Simba kwenye mechi tisa hadi sasa ambapo hajapoteza mchezo wowote
mechi mbili kwenye michuano ya Simba Super Cup (Simba 4-1 Al Hilal, Simba 0-0 TP Mazembe), Ligi Kuu Bara mechi nne (Dodoma 1-2 Simba, Simba 2-2 Azam, Biashara 0-1 Simba na Simba 3-0 JKT Tanzania)
Michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), mechi moja (Simba 3-0 African Lyon), michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mechi mbili (AS Vita 0-1 Simba, Simba 1-0 Al Ahly).
Katika dakika 810, Simba imeruhusu mabao manne huku ikifunga jumla ya mabao 17
Gomes na vijana wake wako nchini Sudan kwa ajili ya majukumu ya Kimataifa kesho Jumamosi wakitarajiwa kushuka dimbani kuikabili Al Merrikh katika mchezo wa ligi ya mabingwa