Simba Queens yapania kuwaadhibu Yanga Princess

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Mar 2021
Simba Queens yapania kuwaadhibu Yanga Princess

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Wanawake 'Serengeti Lite', Simba Queens, jioni ya leo Ijumaa, watashuka pale uwanja wa Uhuru kupepetana na wapinzani wao wa jadi Yanga Princess

Ushindi katika mchezo huu, utairudisha Simba Queens kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo na kuwa katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao

Yanga Princess wanaongoza ligi wakiwa na alama 38 wakati Simba Queens wana alama 36

Timu zote hazijapoteza mchezo msimu huu lakini vijana wa Mussa Mgosi wameahidi kumaliza ubishi wa ipi ni timu bora msimu huu

Afisa Habari wa Simba Haji Manara ambaye yuko nchini Sudan na kikosi cha mabingwa wa nchi, ametuma salamu za ushindi kwa Simba Queens akiwataka mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi uwanja wa Uhuru kuiunga mkono timu yao

Manara amesema kama ilivyokuwa msimu uliopita, hata msimu huu wamejipanga kutwaa kila taji rasmi

"Msimu huu tutashinda mataji yote kuanzia ligi kuu, FA, Ligi ya Wanawake, Ligi ya Vijana, lile la Mapinduzi tuliwaachia kwa sababu tuliombwa," alitamba Manara

"Sisi huku timu iko sawa kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa, tunawatakia kila la kheri Simba Queens washinde. Mashabiki wa Simba tujitokeze kwa wingi uwanja wa Uhuru kuiunga mkono timu yetu"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’