Gomes apania kuwaadhibu waajiri wake wa zamani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Mar 2021
Gomes apania kuwaadhibu waajiri wake wa zamani

Wakati Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba wakiwasili salama nchini Sudan, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Didier Gomes amesema kwa sasa kazi yake kubwa ni kupitia 'mafaili' ya wapinzani wao Al Merrikh ili kufahamu ubora na udhaifu wa kikosi chao

Al Merrikh inatarajia kuikaribisha Simba katika mechi ya Kundi A ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa keshokutwa Jumamosi jijini Khartoum.

Gomes amesema anawafahamu vizuri wapinzani wao kwa sababu aliwahi kuwafundisha kabla ya kujiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha huyo raia wa Ufaransa amesema anaimani mchezo huo wa Jumamosi utakuwa mgumu na ushindani kwa pande zote mbili kwa sababu ya kujiimarisha kwenye msimamo wa kundi hilo.

"Mechi itakuwa ngumu sana kwa sababu wenzetu wamepoteza mechi mbili za kwanza, ninaamini wakiwa nyumbani hawatahitaji kupoteza tena, ninajua hautakuwa mchezo rahisi, lakini sisi tumejipanga kwenda kutafuta matokeo chanya, tunawaheshimu wapinzani wetu tutaingia uwanjani kwa tahadhari kwa ajili ya kupambana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri," alisema Gomes.

Kocha huyo aliongeza kama wachezaji wake wataendeleza kiwango walichokionyesha katika mechi za hivi karibuni, mchezo huo hautakuwa na ushindani na changamoto na watakuwa kwenye nafasi kubwa ya kuchukua pointi tatu.

Mfaransa huyo alimtaja mshambuliaji na nahodha wa timu hiyo, John Bocco amerejea katika ubora wake na ataendelea kumpa dakika 20 katika michezo inayofuata ili kumfanya awe imara siku zijazo huku pia hali ya afya ya golikipa chaguo la kwanza, Aishi Manula imeimarika.

"Alhamdulillah, shukrani kwa dua na sala zenu kwangu, kwani haikuwa rahisi. Ahsante kwa madaktari na wale walionipa huduma ya kwanza baada ya kupoteza fahamu pale kiwanjani," Manula ambaye aliumia katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania alisema.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amesema uamuzi wa kutanguliza maofisa wa timu huko Khartoum unalenga kujiweka katika usalama na itaendelea kufanya hivyo katika kila nchi watakayokwenda kupambana.

“Tulituma maofisa pamoja na baadhi ya viongozi kutoka kwenye benchi letu la ufundi wiki iliyopita na wengine waliondoka jana (juzi) kwa ajili ya kuimarisha usalama, tunajua tunakwenda vitani na lazima tujilinde, kwa kifupi tulitanguliza ujumbe,” alisema Murtaza.

Aliwataja wachezaji 25 ambao wameondoka katika msafara huo kuwa ni pamoja na Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim, Shomary Kapombe, Joash Onyango, Paschal Wawa, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Mohammed Hussein, Jonas Mkude, Rally Bwalya na Mzamiru Yassin.

Nyota wengine ni Luis Miquissone, Hassan Dilunga, Ibrahim Ajib, Clatous Chama, Francis Kahata, Meddie Kagere, Bocco, Tadeo Lwanga, Miraji Athumani, Chriss Mugalu, Peter Muduhwa, Kennedy Juma na David Kameta huku kiungo mshambuliaji 'mtata', Bernard Morrison akiachwa.

Simba imekwenda katika mechi hiyo ikiwa na rekodi nzuri ya kushinda michezo yake miwili iliyotangulia na kuifanya iwe kinara katika Kundi A ikifuatiwa na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Al Ahly zenye pointi tatu kila mmoja wakati Wasudan hao wanaburuza mkia wakiwa hawana pointi hata moja.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’