Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba jioni ya leo wanaianza safari ya kuelekea nchini Sudan wanakokabiliwa na mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Marrikh
Mchezo huo utapigwa siku ya Jumamosi, March 06, saa nne usiku kwa saa za Tanzania
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Simba, imebainisha kuwa Kikosi saa 10:45 jioni kwenda Khartoum, Sudan kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia
Simba ndio vinara wa kundi A wakijikusanyia alama sita baada ya kushinda mechi mbili za kwanza
Wanasaka matokeo ya ushindi nchini Sudan au hata sare na kuhakikisha wanashinda mchezo wa raundi ya nne utakaopigwa jijini Dar es salaam March 16
ADVERTISE HERE