Mabingwa wa nchi Simba kesho Jumatano wanaianza safari ya kuelekea nchini Sudan tayari mwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya El Merrikh ambao utapigwa Jumamosi, March 06, Saa nne usiku
Baada ya mchezo huo, wababe hao wa soka nchini, watarejea Tanzania ambapo March 10 watashuka uwanja wa BenjaminΒ Mkapa kuumana na Tanzania Prisons
Huu ni mchezo wa kisasi kwa Simba, hawa Prisons na pira lao gwaride, walichafua rekodi ya Simba kwenye duru ya kwanza, kipigo kitawahusu hapo kwa Mkapa
March 16 Simba itashuka tena uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Al Merrikh ukiwa ni mchezo wa raundi ya nne michuano ya ligi ya mabingwa
Mechi zote mbili dhidi ya Al Merrikh zina umuhimu mkubwa kwa Simba kwani alama hizo sita zinaweza kutosha kuivusha Simba robo fainali