Kiungo mshambuliaji wa Simba Luis Miquissone jana alitangazwa kuwa mchezaji bora wa wiki wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Nyota huyo raia wa Msumbiji, goli alilofunga kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly limechaguliwa kuwa goli bora la wiki
Miquissone pia amejumuishwa katika kikosi bora cha michuano ya ligi ya mabingwa baada ya mechi za raundi ya pili
Katika kikosi hicho pia yumo beki kisiki Joash Onyango
Ni wiki nzuri kwa Miquissone ambaye jina lake limetajwa sana katika nchi nyingi barani Afrika kutokana na mafanikio aliyopata
Thamani yake imepanda mara dufu, kama Simba itaamua kumuuza leo, basi itavuna 'mkwanja' wa maana
ADVERTISE HERE