Msafara wa kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba utaondoka kesho Jumatano March 03 kuelekea nchini Sudan kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya El Marrikh utakaopigwa Jumamosi, March 06
Mchezo huo una umuhimu wa kipekee kwa Simba kwani matokeo ya ushindi yatawasogeza karibu zaidi ya kufuzu robo fainali
Simba ndio vinara wa kundi A wakijikusanyia alama sita baada ya kushinda mechi zote mbili dhidi ya AS Vita na Al Ahly
Manula kusafiri Sudan
Katika hatua nyingine, mlinda lango namba Aishi Manula anatarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji watakaosafiri kwenda Sudan hapo kesho
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema Manula yuko sawa baada ya kupatiwa matibabu hapo jana alipopata majeraha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania
"Aishi Manula yupo sawa kuwakabili Merekh Jumamosi na inshaallah kesho atasafiri na timu kwenda Sudan kwa ajili ya kipute cha Jumamosi
"Asanteni Wanasimba kwa Dua zenu na Shukran Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya kwa Dr Kairuki kusimamia matibabu ya kipa wa Taifa hili na mabingwa wa nchi," alisema Manara