Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema ana matumaini makubwa kwa mlinda lango wake namba moja Aishi Manula kuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwenda nchini Sudan kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh utakaopigwa Ijumaa ya wiki hii
Manula alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania hapo jana, mchezo ambao uliishuhudia Simba ikiondoka na ushindi mnono wa mabao 3-0
Manula alikimbizwa Hospitalini hapo jana baada ya kupata majeraha hayo, uongozi wa Simba ukisubiri taarifa ya vipimo vyake ili kubaini ukubwa wa majeraha aliyopata na kama anaweza kwenda kucheza kule Sudan au la
"Baada ya mchezo kuisha daktari ameniambia kuwa kila kitu kipo sawa, amepelekwa hospitali kufanyiwa vipimo na tunasubiri majibu. Manula ni mchezaji muhimu sana na nina uhakika ataweza kucheza Sudan," Gomes aliwatoa hofu mashabiki wa Simba