FT : Simba 3-0 JKT Tanzania

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Mar 2021
FT : Simba 3-0 JKT Tanzania

Maafande wa JKT Tanzania wamekimbizwa mchaka mchaka na mabingwa wa nchi Simba katika mchezo wa ligi kuu ambao wamekubali kipigo cha mabao 3-0

Ulikuwa mchezo wa upande mmoja hasa kwenye kipindi cha kwanza Simba ikitawala kwa asilimia 76% na kumaliza kipindi hicho wakiwa mbele kwa mabao mawili

Mnyama Chris Mugalu ndiye aliyeitanguliza Simba kwa bao safi kwenye dakika ya 9 akimalizia krosi murua iliyochongwa na Luis Miquissone

Hilo lilikuwa bao la tano kwa Mugalu kwenye ligi msimu huu

Miquissone aliongeza bao la pili kwenye dakika ya 37 akimalizia pasi murua ya mkongwe Erasto Nyoni

Bao la tatu liliwekwa kambani na nahodha, Papaa John Bocco ambaye huo ni mchezo wake wa pili tangu arejee kutoka kwenye majeraha

Hilo lilikuwa bao lake la tisa sasa akifungana na Meddie Kagere wakiwa vinara wa kuzifumania nyavu

Ni ushindi unaoisogeza Simba karibu kabisa na 'nafasi yake' sasa zikiwa zimesalia alama nne baada ya Machampioni hao wa Tanzania kufikisha alama 45

Baada ya mchezo huo Simba inarejea kwenye mikiki mikiki ya ligi ya mabingwa, wakitarajiwa kusafiri kuelekea nchini Sudan kwa ajili ya mchezo dhidi ya El Merrekh utakaopigwa March 05

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’