Kocha Msaidizi wa Simba Masudi Djuma amesema baada ya kufuzu raundi ya kwanza ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, sasa nguvu zote wamezielekeza kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mbao FC.
Simba itaikaribisha Mbao kwenye uwanja wa Taifa Jumatatu, February 26.
Akizungumza baada ya kuwasili kutoka Djibouti, Djuma amesema kwa sasa hawafikirii mchezo wao wa kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry,kwanza wanahakikisha wanashinda michezo yao ya ligi.
“Kwanza hatuangalii hata huo mchezo wetu na hiyo timu ya Misri, hapa mbele tuna mechi za ligi ambazo ni muhimu kuliko hata hiyo mechi na Al Masri.
“Tunaiandaa timu kwa ajili ya mechi dhidi ya mbao, hiyo Al Masri ukifikika wakati wake tutajiandaa.â€
“Mechi dhidi ya Mbao ni ngumu lakini ni lazima tushinde kwa sababu hakuna kingine tunachoweza kufanya kwa sababu tukitoka sare tunazidi kupoteza nafasi na sisi hatutaki kupoteza nasfai kwa sababu ndio nafasi pekee iliyobaki kwa Simba kushinda ubingwa.â€
Simba inaongoza msimamo wa ligi kuu ya Vodacom ikiwa na alama 42, alama tano zaidi ya Yanga iliyo nafasi ya pili

ADVERTISE HERE