Juzi katika mchezo wa raundi ya tano ya michuano ya kombe la FA dhidi ya African Lyon, nahodha wa Simba John Bocco alicheza kwa takribani dakika tisa akiingia kwenye dakika ya 81 kuchukua nafasi ya Meddie Kagere
Bocco amekuwa nje wa wiki kadhaa tangu alipopata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Fc Platinum ambao Simba ilishinda mabao 4-0
Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes, amesema Bocco atahitaji muda zaidi wa kuimarika kuweza kutumika kwa dakika zote 90
Gomes amesema ataendelea kumrejesha nahodha huyo wa Machampioni hao wa Taifa ili kuhakikisha harudi kwenye majeraha
"Bocco ni mshambuliaji mzuri sana, ni mmoja wa wachezaji ambao nimependa kufanya nao kazi katika klabu ya Simba. Hata hivyo sote tunafahamu, amekuwa majeruhi kwa muda kidogo"
"Nimeanza kwa kumpa dakika chache, nitamuongezea muda siku hadi siku mpaka pale atakapokuwa kamili kuweza kucheza dakika 90"
"Nafurahi anaendelea vizuri, tutarajie kumuona akirejea katika makali yake na kuwa sehemu ya kikosi. Ni mchezaji muhimu anayejituma sana," alisema Gomes