Kahata amwagia sifa Onyango

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Feb 2021
Kahata amwagia sifa Onyango

Kiungo wa Simba Francis Kahata amemwagia sifa beki kisiki Joash Onyango kwa kuonyesha kiwango bora ndani ya kikosi cha mabingwa hao wa nchi

Katika mchezo dhidi ya Al Ahly, Onyango aliiongoza safu ya ulinzi ya Simba kuwadhibiti washambuliaji wa mabingwa hao wa Afrika akicheza sambamba na mkongwe Paschal Wawa

Kocha Mkuu wa Al Ahly Pitso Masemane alimtaja Onyango kuwa ndiye mchezaji aliyemkubali zaidi kwenye mchezo huo pamoja na kuwa alitambua uwezo mkubwa ulioonyeshwa na mfungaji wa bao pekee Luis Miquissone

Kahata ambaye anacheza na Onyango katika timu ya Taifa ya Kenya, amesema tangu amfahamu Onyango, ni mchezaji anayeimarika kila siku

"Namfahamu Onyango, ni mtu asiyependa masihara anapokuwa kazini. Huwa hafanyi makosa ya kizembe, yuko hivyo tangu wakati tukicheza Gor Mahia"

"Nafurahi kumuona anakuwa bora kila uchao. Amekuja hapa Tanzania, moja kwa moja ameingia kwenye kikosi cha kwanza cha Simba, amejihakikishia nafasi na amekuwa mfano wa kuigwa kwenye safu ya ulinzi. Ukitizama kiwango chake, utakubali, Onyango ana msaada mkubwa sana kwa Simba," alisema Kahata

Simba inafukuzia rekodi ya kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa ikiwa kinara wa kundi A mbele ya mabingwa watetezi Al Ahly na wababe wa soka kutoka DR Congo, AS Vita

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’