Waziri aipongeza Simba, Visit Tanzania imetendewa haki

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Feb 2021
Waziri aipongeza Simba, Visit Tanzania imetendewa haki

Waziri wa Utalii na Maliasili, Dk. Damas Ndumaro, amesema Simba imeitendea haki kwa kiwango cha juu jezi yao yenye ujumbe wa 'Visit Tanzania' katika mechi zake za hatua ya makundi ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Simba iliingia makubaliano na serikali kwa kuvaa jezi yenye ujumbe huo kwenye mechi zake baada ya mdhamini wake Sportpesa kukinzana na mdhamini mwingine wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Ndumbaro ametoa kauli hiyo baada ya Simba kupata ushindi mara mbili mfululizo, ugenini dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), na Al Ahly iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Wawakilishi hao wa Tanzania maarufu Wekundu wa Msimbazi walipata ushindi wa bao 1-0 Mjini Kinshasa, DRC juzi wakapata tena ushindi kama huo dhidi ya vigogo wa Afrika kutoka Misri.

Ndumbalo amesema Wizara imefarijika na matokeo hayo waliyopata Simba, kushirikiana na Simba kuhakikisha wanapeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mashindano hayo yanaendelea barani Afrika.

Waziri huyo alisema pia watahakikisha michezo yote inafanya vyema katika mashindano ya kimataifa na kuendelea kutangaza jina la Tanzania vizuri.

"Tunaipongeza sana Simba kwa kazi nzuri waliyofanya, kiukweli wameitendea haki zaidi Visit Tanzania katika mechi zote mbili walizocheza, tutahakikisha wanaendelea kufanya vizuri kwenye michezo inayofuata, na hii haitaishia kwa Simba tu, tunataka kuona michezo yote inafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa," Ndumbaro alisema.

Simba yenye pointi sita ndio inaongoza katika msimamo wa Kundi A ikifuatiwa na Al Ahly yenye pointi tatu sawa na AS Vita huku Al Merrikh ambayo imepoteza mechi zake mbili ilizocheza ikiburuza mkia kwenye kundi hilo.

Baada ya mechi hiyo ya juzi, Simba sasa itasafiri kuelekea Khartoum, Sudan kuwafuata Al Merrikh kati ya Machi 5 na 6, mwaka huu halafu itarejea nyumbani kuwasubiri Wasudani hao.

Mechi itakayofuata itachezwa mapema Aprili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya AS Vita na itamalizia hatua ya makundi nchini Misri dhidi ya Al Ahly

IPP Media

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’