Mamelodi waomba kukodi nyomi la Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Feb 2021
Mamelodi waomba kukodi nyomi la Simba

Jumapili Februari 28, 2021 Mamelodi Sundowns watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili CR Belouizdad kutoka nchini Algeria ukiwa ni mchezo wa ligi ya mabingwa

Mchezo huo unapigwa jijini Dar es salaam baada ya CR Belouizdad ambao ndio wenyeji wa mchezo huo kuomba upigwe nchini kufuatia Serikali ya Algeria kuinyima Mamelodi vibali vya kutua nchini humo kutokana na changamoto ya corona

Jana viongozi waandamizi wa Mamelodi walikuwepo uwanja wa Benjamin Mkapa wakiishuhudia Simba, mabingwa wa nchi wakiwaadhibu vikali Al Ahly kwa kuwachapa bao 1-0 katika mchezo ambao Al Ahly hawatausahau kutokana na 'pira biriani' walilokutana nalo kutoka kwa vijana wa Didier Gomes

Kama ilivyo kawaida, ushindi wa Simba ulichagizwa na mashabiki wake takribani 30,000 walioruhusiwa kushuhudia mchezo huo

Sasa baada ya mchezo viongozi hao wa Mamelodi wakamvaa Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez wakiomba sapoti kutoka kwa Simba katika mchezo wao wa Jumapili

"Hongera sana kwa ushindi leo, nasi tutakuwa uwanjani hapa Jumapili. Tunaomba uwaambie mashabiki wenu waje watuunge mkono katika mchezo wetu," Afisa wa Mamelodi alisikika akiongea na Barbara

Simba kupitia Mtendaji wake Mkuu Barbara, ikaahidi kuwa nao bega kwa bega huku Barbara akiwaachia mawasiliano yake kwa ajili ya majadiliano zaidi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’