Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes ameeleza kufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya vigogo wa soka Barani Afrika Al Ahly, Simba ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa hapo jana
Gomes amesema kwa jinsi walivyocheza mchezo huo, walikuwa bora zaidi ya wapinzani wao na walipata ushindi waliostahili
"Nawapongeza wachezaji wangu kwa ushindi huu muhimu. Nadhani tulikuwa bora, tulicheza vizuri kwa muda mwingi ingawa zipo nyakati tulipoteza umakini. Ni ushindi ambao tulistahili," alisema Gomes
"Tumeshinda mechi mbili na tunaongoza kundi A, ni matokeo muhimu sana kwetu. Tunaanza maandalizi ya mchezo unaofuata (dhidi ya Al-Marreik) wiki mbili zijazo. Hautakuwa mchezo mwepesi hii ni timu ninayoifahamu vizuri"
Al Marreikh wanaburuza mkia baada ya kupoteza mechi zote mbili za kwanza
Jana walibugizwa mabao 4-1 na AS Vita huko Sudan na mchezo unaofuata March 05 wanakutana na Simba hukohuko kwao