Tangu atue klabu ya Al Ahly, kocha Pitso Mosimane hakuwa amepoteza mchezo wowote ndani ya bara la Afrika
Mchezo pekee waliokuwa wamefungwa ni dhidi ya Bayern Munich kwenye michuano ya vilabu bingwa duniani iliyofanyika mapema mwezi huu Qatar
Simba inakuwa timu ya kwanza kuifunga Al Ahly chini ya kocha Mosimane anayetajwa kuwa bora zaidi barani Afrika kwa sasa
Lakini zaidi, bao la Simba limefungwa na Luis Miquissone aliyewahi kufanya kazi na Mosimane misimu miwili nyuma

Ndio, wakati Mosimane akiwa kocha wa Mamelodi Sundowns, Miquissone alikuwa mmoja wa wachezaji wa timu hiyo
Hata hivyo Mosimane hakuwa akimpa Miquissone nafasi ya kutosha katika kikosi chake, kwa misimu miwili ya mwisho alimtoa kwa mkopo klabu ya UD Songo kabla ya Simba kufika mezani kumsajili
Ilikuwa faraja sana kwa Miquissone kufunga bao pekee la ushindi wa Simba leo dhidi ya mtu ambaye hakuwa akimuamini
Miquissone alipambana sana katika mchezo dhidi ya Al Ahly, hakika alikuwa na jambo lake, na amelifanikisha