Kapombe alipumzishwa tu mechi dhidi ya Gendarmerie

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
22 Feb 2018
Kapombe alipumzishwa tu mechi dhidi ya Gendarmerie
Katika mchezo wa marudiano kati ya Gendarmerie dhidi ya Simba, beki Shomari Kapombe aliachwa nje ya kikosi na hivyo kuzua hofu kwa baadhi ya mashabiki waliodhani amarejea tena kwenye majeruhi.

Lakini ukweli ni kwamba kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre aliamua kumpumzisha tu baada ya kumtumia katika michezo mitano mfululizo.

Kabla ya kurejea dimbani mwezi January, Kapombe alikaa nje kwa zaidi ya miezi sita akiuguza majeraha ya goti na mgongo.

Lechantre amebainisha kwamba aliamua kumuweka benchi Kapombe kwa kuwa amechoka, baada ya kucheza mechi nyingi mfululizo.

“Niliongea naye kabla ya mchezo, nikamwambia umechoka, umetoka kwenye majeruhi na umecheza mechi tano ngumu mfululizo, hivyo umechoka,” alisema Lechantre.

Kapombe alipewa mapumziko ili kupata muda mzuri wa kujiandaa na mashindano ya Ligi Kuu na mechi ijayo dhidi ya Al Masry ya Misri.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →