Baraza aitabiria ushindi Simba, atoa tahadhari

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
23 Feb 2021
Baraza aitabiria ushindi Simba, atoa tahadhari

Kocha Mkuu wa Biashara United Francis Baraza amesema kikosi cha Simba kina uwezo wa kupata matokeo chanya mbele ya Al Ahly ikiwa watacheza kwa nidhamu na utulivu mkubwa.

Leo Simba ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Al Ahly ya Misri. Mchezo ukitarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 jioni na mashabiki 30,000 watapata fursa ya kushuhudia ndani ya Uwanja wa Mkapa 

Baraza ambaye hivi karibuni timu yake ilichezea kichapo kutoka kwa Simba kwa kufungwa bao 1-0 kule Musoma, amesema kikosi cha Simba kiko vizuri na leo wanaweza kupata matokeo dhidi ya Al Ahly

"Simba wameanza vizuri na wanaweza kupata matokeo chanya , ila lazima waongeze nidhamu ndani ya uwanja na kupunguza makosa yasiyo ya lazima hasa kwa mabeki pamoja na viungo"

"Ikiwa watakuwa wanaruhusu makosa iwe ndani ya 18 ama karibu na 18 ni hatari kwao kwa kuwa wapinzani wao wanaweza kutumia kila nafasi na kugeuza kuwa bao, hapo umakini unahitaji," alisema Baraza 

Huu ni mchezo unaozikutanisha timu ambazo zimeonyesha ubora katika michezo yao ya kwanza, Simba ikiifunga AS Vita bao 1-0 ugenini huku Al Ahly ikipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Al Marreikh kule Misri

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
30m ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →