Kwa Mashabiki wa Simba leo ni siku muhimu sana kwani wataishuhudia timu yao ikishuka katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Al Ahly katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika
Ni mchezo wa kibabe utakaowakutanisha mabingwa, Simba ikihitaji alama tatu muhimu kujiweka katika mazingira mazuri ya kuvuka kwenda robo fainali
Huu ni mchezo ambao utafuatiliwa sio hapa Tanzania tu, Bara zima la Afrika macho yote yatakuwa hapa nchini
Al Ahly ndio klabu kongwe na yenye historia ya kipekee barani Afrika. Hapa tunawazungumzia mabingwa wa kihistoria wa michuano hii ya ligi ya mabingwa, wameshinda kombe hili mara tisa
Ndio klabu iliyotwaa mataji mengi DUNIANI na hata ukizungumzia idadi ya mashabiki, Al Ahly wana mashabiki wengi sana
Wanachuana na Simba ambayo nayo imejipambanua kutokuwa na masihara wanapocheza katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Al Ahly walichezea kichapo cha bao 1-0 walikuja nchini mwaka juzi, Wanamsimbazi wameapa, leo tena lazima mabingwa hao watetezi waache alama zote tatu
Sapoti ya mashabiki ni silaha muhimu kwa Simba leo, bila shaka tiketi zote 30,000 zitauzwa, mpaka kufikia jana jioni tiketi za VIP A zilikuwa zimemalizika
Mafanikio ya Simba katika mchezo huo ni mafanikio ya nchi. Kwani kufanya vizuri kwa Simba kutaihakikishia Tanzania uwakilishi wa vilabu vinne kwenye michuano ya CAF msimu ujao
Hivyo dua za Watanzania wazalendo ni muhimu sana siku ya leo kuona Simba inashinda mchezo
Hii ni mechi ya mabingwa, ni mechi ya kulinda heshima na Simba hapa Tanzania na hii ni mechi ya kupeperusha bendera na kuitangaza Tanzania Kimataifa
Kila la kheri Simba, Kila la kheri mabingwa wa nchi