Droo ya hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) imefanyika leo jijini Cairo huko Misri ambapo wawakilishi wengine wa Tanzania, Namungo Fc watakuwa kundi D kama watafanikiwa kufuzu makundi
Namungo wanahitaji ushindi, sare au kufungwa sio zaidi ya mabao 4-0 katika mchezo wa pili dhidi ya 1 de Agosto utakaopigwa Jumatano ijayo uwanja wa Azam Complex
Raja Casablanca, Pyramids na Nkana Fc ndizo timu nyingine zilizopangwa kundi D
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Namungo Fc kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo
Lakini pia ni historia nzuri kwao kwani wanakaribia kufikia hatua hiyo msimu mmoja tu tangu wapande daraja kutoka ligi daraja la kwanza
Ni heshima kubwa kwa Tanzania kuwa na timu mbili kwenye hatua ya makundi ya michuano ya vilabu barani Afrika
Mabingwa wa nchi Simba wao wanaendelea kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kesho wakishuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Al Ahly