Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema wameiandaa timu kikamilifu kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly utakaopigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam
Akizungumza na Wanahabari katika Mkutano uliofanyika ndani ya uwanja huo mapema leo, Matola amesema wanafahamu mchezo hautakuwa mwepesi lakini lengo lao ni kushinda
"Tumejipanga, tumewaandaa wachezaji kikamilifu kuhakikisha tunaweza kufanikisha mpango tuliojiwekea. Ni mechi ngumu lakini tumejipanga kupata matokeo mazuri nyumbani," alisema Matola
Aidha, nahodha wa Simba, John Bocco anasema wachezaji wako tayari kupambana na kufuata maelekezo ya mwalimu watakayopata kwenye mazoezi yao ya mwisho yanayofanyika leo
"Tunawaheshimu wapinzani wetu, ni timu kubwa Afrika lakini kwa mbinu tutakazoingian azo kesho, naamini tutapata ushindi", amesema John Bocco huku akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuwaamini wachezaji wao
Mchezo utapigwa kuanzia saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa