Tutawakabili Al Ahly na tahadhari - Gomes

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Feb 2021
Tutawakabili Al Ahly na tahadhari - Gomes

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema wachezaji wake wataendeleza nidhamu ya kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza kwenye mchezo wa pili wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, Kesho jioni

Simba wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kutoka kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo wa kwanza wa ugenini dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo sawa na Al Ahly wanaongoza kundi hilo baada kuibuka na mabao 3-0 dhidi ya Al Merrikh ya Sudan

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Gomes alisema hakuna mchezo rahisi kwenye hatua hiyo nidhamu ya kumuheshimu mpinzani ni lazima.

"Tunaenda kucheza na Al Ahly mabingwa watetezi wanawachezaji wenye mbinu na wanafanya vizuri, lakini kwetu tunayonafasi ya kujipanga kulinda ushindi sioni kama kunambinu zaidi ya kuongeza nidhamu katika kuzuia mashambulizi yao" alisema Gomes

Gomes amesema wachezaji wake wanaendelea vyema na uzuri wapo kwenye kipindi kizuri baada ya kuanza vyema ugenini na safari hii watakuwa nyumbani mipango yao ni kuendeleza wimbi la ushindi kujitengenezea mazingira mazuri kwenye kundi hilo.

Simba watacheza mchezo huo na Al Ahly ambao ni mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo wakiwa na kumbukumbu ya kutoka kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa hatua kama hiyo msimu wa mwaka juzi.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’