Katika mazoezi ya jana, viongozi wa Simba wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' walikuwemo ndani ya dimba la Benjamin Mkapa kuwashuhudia vijana wakikamilisha maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Al Ahly hapo kesho
Hakika hii itakuwa mechi kihistoria, Simba imefanya maandalizi makini hao Al Ahly lazima 'wapasuke' uwanja wa Benjamin Mkapa kesho
Huu ni uwanja wetu, hakuna anayeweza kuondoka na alama tatu hapo mbele ya Simba
Mo amewataka wachezaji wahakikishe alama zote tatu zinabaki Dar na zaidi ni kuwa wakishinda mchezo huo, kama kawaida wataondoka na 'mkwanja' wa maana




ADVERTISE HERE