Namungo Fc yanusa makundi Shirikisho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Feb 2021
Namungo Fc yanusa makundi Shirikisho

Wakati Machampioni wa nchi Simba wakisubiri kuonyesha shoo ya kibabe dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Jumanne, Wawakilishi wengine wa nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho, Namungo Fc wanakaribia kuandika historia ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza

Ni baada ya ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya CD De Agosto ya Angola katika mchezo wa kwanza wa mtoano uliopigwa uwanja wa Azam Complex jioni ya leo

Katika mchezo huo CD De Agosto walikuwa wenyeji. Baada ya Namungo kufanyiwa figisu kule Angola, CAF iliagiza mechi zote mbili kupigwa jijini Dar es salaam

Hivyo ushindi waliopata Namungo leo ni wa ugenini, CD De Agosto watahitaji kushinda mabao 5-0 kuweza kupindua matokeo kwenye mchezo wa pili ambao pia utapigwa Azam Complex

Haya ni mafanikio makubwa kwa soka la Tanzania kwani kwa mara ya kwanza tunakwenda kuwa na timu mbili hatua ya makundi katika michuano Afrika

Hata hivyo Namungo wanapaswa kumalizia ngwe ya pili kabla ya kuanza kushangilia

Lakini kwa matokeo ya leo wanastahili pongezi...!

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’