Al Ahly hawachomoki kwa Mkapa - Zimbwe Jr

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Feb 2021
Al Ahly hawachomoki kwa Mkapa - Zimbwe Jr

Nahodha Msaidizi wa Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema wamejipanga kuikabili Al Ahly katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika ambao utapigwa keshokutwa Jumanne

Zimbwe Jr amesema kila mchezaji anafahamu umuhimu wa ushindi katika mchezo huo, ari ya kila mmoja iko juu na wanaamini watapata matokeo chanya

Al Ahly waliwasili Tanzania usiku wa kuamkia jana tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kushuhudiwa na mashabiki takribani 30,000 kulingana na maelekezo yaliyotolewa na Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF)

"Morali ya wachezaji ni kubwa na kila mmoja anahitaji ushindi hivyo tutapambana kupata matokeo mazuri mbele ya Al Ahly"

"Kila mmoja wetu anajua kwamba ushindani ni mkubwa, tunahitaji kufanya vizuri kwenye mechi zetu za kitaifa na kimataifa hivyo mashabiki waje kwa wingi uwanjani kutupa sapoti," amesema Zimbwe Jr

Al Ahly ndio vinara wa kundi A wakitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na Simba huku timu zote zikiwa na alama tatu

Al Ahly waliifumua Al Marreikh mabao 3-0 nchini Misri wakati Simba ilichomoza na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya AS Vita

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’