Nahodha John Bocco ni miongoni mwa wachezaji walioshiriki mazoezi ya Simba kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa keshokutwa Jumanne
Bocco amekuwa nje kwa wiki kadhaa baada ya kupata majeraha katika mchezo ulioipa Simba tiketi ya kuingia makundi wakishinda mabao 4-0 dhidi ya Fc Platinum jijini Dar es salaam
Kurejea kwake kunazidi kuimarisha safu ya ushambuliaji kuelekea mchezo huo ambao Simba inahitaji kuondoka na ushindi
Katika mchezo uliopita dhidi ya Al Ahly, Bocco ndiye aliyetengeneza bao la Simba lililofungwa na Meddie Kagere 'MK-14'
Simba sasa inaelekea katika mchezo huo ikiwa silaha zake zote
ADVERTISE HERE