Mabingwa watetezi ligi ya mabingwa barani Afrika, Al Ahly wamewasili nchini kuelekea mchezo wao dhidi ya Machampioni wa Tanzania klabu ya Simba
Mchezo utapigwa Jumanne, Februari 23 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, saa kumi kamili jioni
Al Ahly wamewasili nchini wakiwa na kikosi cha wachezaji 22
Wakati wapinzani wao wakitua, Simba waliingia moja kwa moja kambini wakitokea mkoani Mara kukamilisha mchezo wa ligi kuu dhidi ya Biashara United
Huu ni mchezo muhimu sana kwa Simba, matokeo ya ushindi yatawaweka mabingwa hao wa nchi katika nafasi nzuri zaidi ya kutinga robo fainali kwani kimahesabu watahitaji angalau alama nyingine tatu kutoka michezo minne
ADVERTISE HERE